Matthew 28

1Baadaye jioni siku ya Sabato, jua lilipokuwa likichwa kuelekea siku ya kwanza ya juma, Mariamu magadalena, na yule Mariam mwingine walikuja kuliona kaburi. 2Tazama kulikuwa na tetemeko kubwa, kwa sababu malaika wa Bwana alishuka na kulivingirisha lile jiwe, kisha akalikalia.

3Sura yake ilikuwa kama ya umeme, na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji. 4Wale walinzi walijawa na hofu na kuwa kama wafu.

5Yule malaika akawafafanulia wale wananawake akisema, “msiogope kwa maana najua kuwa mnamtafuta Yesu, aliyesulibiwa. 6Hayupo hapa, lakini amefufuka kama alivyowaambia. Njooni muone mahali ambapo Bwana alilala. 7Nendeni haraka mkawaambie wanafunzi wake, ‘Amefufuka toka wafu, tazama amewatangulia Galilaya. Huko ndiko mtamwona.’ Tazama mimi nimewaambia.”

8Wale wanawake waliondoka pale kaburini haraka wakiwa na hofu na furaha kubwa, na wakakimbia kuwaambia wanafunzi wake. 9Tazama Yesu akakutana nao na kusema, “Salamu.”wale wanawake walikuja na kushika miguu yake, na kisha wakamwabudu. 10Kisha Yesu akawaambia, “msiogope, nendeni mkawaambie ndugu zangu watangulie Galilaya. Huko wataniona.

11Wakati wale wanawake walipokuwa wakienda, tazama baadhi ya walinzi walienda mjini na kuwaambia wakuu wa makuhani mambo yote yaliyokuwa yametokea. 12Nao makuhani walipokuwa wamekutana na wazee na kulijadili jambo hilo pamoja nao, walitoa kiasi kikubwa cha pesa kwa wale askari 13na kuwaambia, “Waambieni wengine kuwa, ‘wanafunzi wa Yesu walikuja usiku wakauiba mwili wa Yesu wakati sisi tulipokuwa tumelala.’

14Kama taarifa hii itamfikia liwali, sisi tutamshawishi na kuwaondoleeni ninyi mashaka yote.” 15Kwa hiyo wale askari wakazichukua zile pesa na kufanya kama walivyokuwa wameelekezwa. Habari hii ikaenea sana kwa Wayahudi na imekuwa hivyo hadi leo.

16Lakini wale mitume kumi na mmoja walienda Galilaya, kwenye ule mlima aliokuwa amewaelekeza. 17Nao walipomwona, walimwabudu. lakini baadhi yao waliona shaka.

18Yesu akaja kwao akawambia akisema, “Nimepewa mamlaka yote duniani na mbinguni. 19Kwa hiyo enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi. Wabatizeni katika jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtatkatifu.

20Wafundisheni kuyatii mambo yote niliyowaamuru, Na tazama, mimi niko pamoja nanyi daima, hata mpaka mwisho wa dunia.

Copyright information for SwaULB